Kila kitu kinahusiana na kutaka


Swali: Mimi ni mwanafunzi nasoma lugha Uingereza. Huko niliko hakuna sehemu ya kuswali. Je, inajuzu kwangu kukusanya swalah?

Jibu: Hapana. Kukusanya swalah haijuzu. Swali sehemu yoyote unayoweza, sawa uko na wengine au uswali peke yako. Utapata sehemu ya kuswalia – Allaah akitaka. Kila kitu kinahusiana na kutaka. Ikiwa kweli mnataka basi Allaah atakufanyieni wepesi.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Liqaa'-ul-Jumu´ah bit-Twaa'if http://alfawzan.af.org.sa/ar/node/17101
  • Imechapishwa: 24/09/2017