Swali: Wako watu ambao wanawatolea salamu mama wa jirani yake ambaye tayari ni mtumzima ambaye ameshafikisha miaka sabini au chini kidogo ya hapo. Huenda wakati mwingine anambusu kichwa chake ana akasema kwamba hakuna ubaya kufanya hivo kwa sababu ni katika kumfanyia heshima mwanamke huyu ambaye hamtamani. Je, kitendo cha huyu kinafaa?

Jibu: Kuhusu kumtolea salamu inafaa. Inafaa akamtolea salamu bibi kizee wa jirani yake kutokana na ule ukaribu ulio kati yao na kwa sababu Allaah (Ta´ala) amesema:

وَالْقَوَاعِدُ مِنَ النِّسَاءِ اللَّاتِي لَا يَرْجُونَ نِكَاحًا فَلَيْسَ عَلَيْهِنَّ جُنَاحٌ أَن يَضَعْنَ ثِيَابَهُنَّ غَيْرَ مُتَبَرِّجَاتٍ بِزِينَةٍ

“Na wale wanawake wazee waliokatika hedhi ambao hawataraji kuolewa, basi hapana neno juu yao kupunguza baadhi ya nguo zao bila ya kudhihirisha mapambo yao.”[1]

Kuhusu kumbusu kichwa na kupeana naye mikono haijuzu. Kwa sababu mambo ni kama wanavosema wenyewe: kila chenye kutupwa kuna mwenye kukiokota. Yeye hata kama hamtamani, lakini atambue kuwa shaytwaan hupita ndani ya mifupa ya mwanadamu kama damu. Inatosha kumsalimia, muulize juu ya hali yake na hali ya watoto wake pasi na kuwa naye faragha na hapo hakuna dhambi kwake.

[1] 24:60

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Liqaa’ ash-Shahriy (47) http://binothaimeen.net/content/1077
  • Imechapishwa: 05/07/2020