Swali: Umetaja mifumo ya kale miongoni mwa Murji-ah, Qadariyyah na Khawaarij. Halafu ukaongezea juu ya hilo kwa kusema na mifumo ya leo. Tunaomba utueleweshe ni mifumo yepi hiyo na khatari yake katika jamii?

Jibu: Nyinyi mnaijua. Kila ambao unaenda kinyume na mfumo wa Salaf, basi ni miongoni mwa mifumo inayoenda kinyume. Hakuna haja ya kulenga mfumo fulani. Ninawapa kidhibiti na mtakipachika kwenye mifumo hii: yule ambaye anaenda kinyume na mfumo wa Salaf, achaneni naye. Na yule anayeafikiana nao, shikamaneni naye.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh ´Aqiydat-is-Saffaariniyyah (15) http://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/sfranih_15.mp3
  • Imechapishwa: 14/06/2018