Kikwikwi kinachomtoka mtu baada ya kula sana kinafunguza?

Swali: Alfajiri katika Ramadhaan mfungaji anakuwa na tumbo lenye kujaa. Pindi anapotaka kutoa hewa kunatoka kitu katika chakula au maji kidogo ambayo hayafiki kooni. Je, kunafunguza?

Jibu: Haya uliyoelezea huwatokea watu wengi pindi matumbo yao yamevaa chakula. Mtu anapofanya kikwikwi kunaweza kutoka kitu katika chakula na maji. Ikiwa hakikufika kinywani na hakukimeza hakuna neno.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (19/232)
  • Imechapishwa: 12/06/2017