Kikuku dhidi ya ugonjwa wa damu

Swali: Ni ipi hukumu ya kuvaa kicheni cha mkono kwa ajili ya kutibu ugonjwa wa damu?

Jibu: Dawa ni sababu ya ponyo na mwenye kusababisha upone ni Allaah (Ta´ala). Kwa hivyo hakuna sababu isipokuwa ile ambayo imefanywa na Allaah kuwa ni sababu na ile sababu ambayo imefanywa na Allaah kuwa ni sababu. Sababu zimegawanyika sampuli mbili:

1- Sababu iliowekwa katika Shari´ah kama vile Qur-aan Tukufu na du´aa. Kama alivosema Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) juu ya “al-Faatihah”:

“Ni kipi kimekujuza kuwa ni mtabano?”[1]

 Vilevile Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alikuwa akiwasomea wagonjwa wa kuwaombea du´aa na hivyo Allaah akamponya yule ambaye Allaah ametaka kumponya.

2- Sababu zinazohisiwa kama mfano wa dawa za mwili, kukiwemo asali, au dawa zilizojaribiwa. Aina hii ni lazima iwe na athari ya wazi na sio iwe kwa njia ya kudhani na kufikiria. Dawa hii ikithibiti kuwa iko na taathira ya wazi au inayohisiwa, basi itasihi kufanywa kuwa dawa ambayo kwayo inapatikana ponyo kwa idhini ya Allaah. Ama ikiwa ni kwa njia tu ya kudhani na kufikiria ambayo inamfanya mgonjwa kufikiria na hivyo akapata raha ya kinafsi na hivyo maradhi kweli yakaondoka, basi hiyo haijuzu kuitumia wala kuthibitisha kuwa ni dawa ili mtu asije kuingia kwenye mambo ya kufikiri na kudhania. Kwa ajili hiyo imekatazwa kuvaa pete na vicheni kwa ajili ya kuondosha au kuzuia maradhi, kwa sababu hiyo sio sababu iliyowekwa na Shari´ah wala sababu inayohisiwa. Kitu ambacho hakikuthibitishwa kuwa ni sababu iliyowekwa katika Shari´ah wala yenye kuhisiwa basi haitofaa kufanywa kuwa ni sababu. Kile kitendo cha kuifanya kuwa sababu ni aina fulani ya kukinzana na Allaah katika ufalme na kumshirikisha, kwani Allaah (Ta´ala) pekee ndiye Mwenye kuweka sababu. Shaykh-ul-Islaam Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab (Rahimahu Allaah) ameandika mlango mzima kuhusiana na mada hii katika “Kitaab-ut-Tawhiyd”. Sifikiri kuwa kicheni hicho cha mkono dhidi ya ugonjwa wa damu alichopewa kutoka katika dula la madawa kinaingia katika sampuli hii. Kwani kicheni hicho cha mkono sio sababu ya kidini wala inayohisiwa dhdi ya ugonjwa wa damu inayomfanya kupona. Kwa ajili hiyo haifai kwa yule aliyesibiwa kutumia kikuku hicho mpaka atambue kweli kuwa hiyo ni sababu inayopelekea kupona.

[1] al-Bukhaariy (2276) na Muslim (2201).

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (17/69-70)
  • Imechapishwa: 11/08/2021