Swali: Kuna mwanamke aliye na umri wa miaka sabini anataka kuhiji na kuja Makkah pasi na Mahram. Ni ipi hukumu?

al-Fawzaan: Anatokea wapi?

Jibu: Tunisia.

al-Fawzaan: Hapana, haijuzu. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Si halali kwa mwanamke anayemwamini Allaah na siku ya Mwisho kusafiri isipokuwa awe pamoja naye Mahram.”

Haijalishi kitu sawa iwe Tunisia au kwenginepo. Haijalishi kitu sawa iwe ni hajj au kwenginepo. Ikiwa hana Mahram yoyote basi awakilishe mtu amuhijie.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Tafsiyr-ish-Shaykh Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab (13) http://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/tf–1432-08-09.mp3
  • Imechapishwa: 27/05/2018