Swali: Ni kipi kinachozingatiwa katika kikomo cha ujirani au ni jambo linarudi katika desturi za watu?

Jibu: Hapana. Ukaribu wa milango miwili. Kila ambavo mlango unakuwa karibu basi anakuwa na haki zaidi.

Swali: Lakini kikomo ni kipi?

Jibu: Kumepokelewa juu ya hilo nyumba arobaini. Lakini sijui Hadiyth yoyote Swahiyh inayoweka kikomo. Kila ambavyo jirani atakuwa karibu basi ana haki zaidi ya kufanyiwa wema. Nakusudia kila ambavyo mlango wake utakuwa karibu zaidi nawe.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/21703/ما-الضابط-المعتبر-في-تحديد-الجوار
  • Imechapishwa: 24/09/2022