Swali: Mimi ni kijana mwenye miaka 21 ambaye nataka kuoa. Lakini familia yangu inanikatalia na kunambia bado mdogo japokuwa naweza kusimamia majukumu ya ujumba. Wanatumia hoja ya kwamba nyuma yangu nina ndugu wawili ambao ni lazima kwanza waoe wao halafu mimi ndio nioe baada yao. Pamoja na kuwa ndugu zangu hawataki kuoa. Nifanye nini; niwatii wazazi wangu au nifanye nini?

Jibu: Ninamwambia ndugu muulizaji ya kwamba si mdogo. Ambaye umri wake ni miaka 21 sio mdogo kwa kuoa.

´Amr bin al-´Aasw (Radhiya Allaahu ´anh) alioa akiwa na miaka 11 na akapata mtoto. Kwa ajili hii inasemwa kwamba yeye na mwanae ´Abdullaah wanapishana miaka 13. Yaani baina ya baba na mtoto. Ninamwambia muulizaji kwamba amtegemee Allaah na aoe na kwamba si mtoto.

Kuhusu ndugu zako wawili waliokutangulia pale itapowakuwia usahali wataoa. Hili ni kosa kubwa walilonalo baadhi ya watu ambapo hawakumuozesha msichana mdogo kwa sababu mkubwa wake bado hajaolewa! Hili ni haramu kwao. Anapochumbiwa na kijana mwenye kuridhiwa dini na tabia yake wamuozeshe. Huenda kuolewa kwa binti huyu mdogo ikawa ndio sababu ya kuolewa huyu mkubwa. Mara nyingi anapoolewa msichana mdogo anamfungulia mlango yule mkubwa. Hili ni jambo linalojulikana.

Tumesimuliwa mara nyingi mtu anaoa na kukaa miaka kumi na tano au kumi na sita na mke asiyezaa, kisha anaoa ambapo yule mke wa pili anashika mimba katika ule usiku wa kwanza na yule bi mkubwa anashika ujauzito siku ile ile pamoja na kuwa alikuwa na mume wake miaka mingi pasi na kuzaa. Msichana huyu huenda Allaah akawafungulia mlango dada zake wakubwa na vivyo hivyo mvulana huenda Allaah akawafungulia mlango kaka zake.

Kwa hivyo mimi namwambia ndugu muulizaji aoe na amtake msaada Allaah.  Hilo halizingatiwi kuwa ni kuwaasi wazazi wawili na wala halizingatiwi kuwa ni kukata udugu na wale ndugu wawili kabisa.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Liqaa’ ash-Shahriy (15)
  • Imechapishwa: 01/10/2017