Kijana anayeishi na wazazi wake anatoa au anatolewa Zakaat-ul-Fitwr?

Swali: Mimi ni kijana ninaishi na baba na mama yangu na bado sijaoa. Je, Zakaat-ul-Fitwr yangu natolewa na baba yangu au natoa kwa mali yangu binafsi?

Jibu: Zakaat-ul-Fitwr ni wajibu na faradhi. Ibn ´Umar (Radhiya Allaahu ´anhumaa) amesema:

“Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amefaradhisha Zakaat-ul-Fitwr pishi[1] ya tende au pishi ya shayiri kwa mdogo na mkubwa, muungwana na mtumwa, mvulana na msichana katika waislamu.”

Ni kama mambo mengine ya wajibu ambayo anaambiwa kila mmoja kivyake. Wewe ndiye mwenye kusemezwa na hivyo unatakiwa kujitolea zakaah kivyako hata kama uko na baba na kaka. Vilevile mke ni mwenye kusemezwa na hivyo anatakiwa kujitolea zakaah kivyake hata kama yuko na mume.

Lakini mkuu wa familia akitaka kuitolea familia yake zakaah hakuna neno kufanya hivo. Ikiwa mtu huyu yuko na baba ambaye anamuhudumia na akapenda kumtolea zakaah mwanae hakuna neno kufanya hivo.

[1] Ibn Baaz (Rahimahullaah) amesema: ”Pishi  moja ni sawa na takriban 3 kg.” (Majmuu´-ul-Fataawaa (14/201))

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (18/261)
  • Imechapishwa: 21/06/2017