Swali: Ni ipi hukumu ya kuweka kifaa cha umeme kinacholeta joto mbele ya waswaliji wakati wako wanaswali? Je, kuna makatazo ya Kishari´ah yaliyopokelewa juu ya hilo?

Jibu: Hakuna neno kuweka kifaa cha umeme kinacholeta joto upande wa Qiblah wa msikiti mbele ya waswaliji. Sijui juu ya jambo hilo makatazo yoyote ya Kishari´ah.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaa Arkaan-il-Islaam, uk. 344
  • Imechapishwa: 09/05/2020