Swali: Ni upi mpaka wa mwanamke kutoka kwa ajili ya kuwatembelea ndugu zake? Ni ipi hukumu ya mwanamke kwenda sokoni? Inajuzu kwa mtoto wake wa kiume kumkatalia kumpeleka mama yake sokoni?

Jibu: Kadri ambavyo mwanamke atatulizana nyumbani kwake ndio bora zaidi. Leo anaweza kufanya matembezi kwa njia nyepesi ilihali yuko nyumbani kwake. Hilo linakuwa kwa njia ya simu. Kwa njia hii mtu anaweza kuwasiliana na ndugu zake mara mbili kwa siku. Lakini kukiwepo haja ya kufanya matembezi, kwa mfano kumtembelea ndugu yake ambaye amegonjweka au mfano wa hayo, amtembelee. Lakini hata hivyo anatakiwa asiwe mwenye kuonesha mapambo, asijitie manukato, atembee mwendo wa mwanamke mwenye haya na ajitenge mbali na mionekano ya fitina.

Kuhusu mwanamke kwenda sokoni peke yake hakuna neno. Lakini asiwe ni mwenye kujitia manukato wala mwenye kuonesha mapambo. Pamoja na haya yote bora zaidi ni yeye kutoenda sokoni na badala yake amwambie yale mahitajio anayoyataka mume wake, kaka yake au mtoto wake wa kiume amnunulie nayo na kumletea. Ikiwa ni lazima aende kujinunulia mwenyewe ni sawa. Kwa sharti kuaminike kutowepo fitina. Lakini lau ataenda na mmoja katika Mahaarim zake ndio bora zaidi. Hili halina shaka.

Mama akimuomba mvulana wake kumsindikiza sokoni na kutoka huku ikawa kwa sura iliyoruhusiwa, kumtii kwa kwenda pamoja nae ni sehemu katika kumtendea wema. Katika kufanya hivo kunapatikana kwanza kumtii na pili kumlinda na michezo.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Liqaa’ ash-Shahriy (11)
  • Imechapishwa: 03/05/2020