Sifa za Allaah zimegawanyika aina mbili:

1 – Sifa za dhati.

2 – Sifa za kimatendo.

Sifa za kidhati kidhibiti chake ni kwamba haziachani na Mola. Kwa mfano wa hayaa, elimu, uwezo, usikivu na kuona.

Sifa za kimatendo ni zile ambazo zimefungamana na matakwa na utashi. Kwa mfano kushuka, kulingana [al-Istiwaa´], kuhuisha, kufisha, kuridhia, kughadhibika, kuchukia, kukasirika na nyinginezo katika sifa za kimatendo.

  • Mhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah ar-Raajihiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Hidaayah ar-Rabbaaniyyah fiy Sharh al-´Aqiydah at-Twahaawiyyah (01/74)
  • Imechapishwa: 31/05/2020