Kidhibiti cha anayemkusudia Allaah na anayekusudia dunia

Swali: Imamu anachukua mshahara kwa ajili ya kuswalisha. Je, anaingia miongoni mwa wale wanaokusudia kwa matendo yao manufaa ya kidunia? Ni vipi mwanafunzi atasalimika kuikusudia dunia kwa kitendo chake?

Jibu: Mimi nimekwishakupeni kidhibiti juu ya hili: kazi ya uadhini, uimamu, kujifunza elimu, kupambana Jihaad katika njia ya Allaah, Hajj na ´Umrah, ikiwa makusudio ya mtu ni kuchukua mali peke yake, basi huyu amekusudia kwa kitendo chake manufaa ya kidunia. Naye anaingia katika makemeo haya makali[1]. Ama ikiwa makusudio yake ni ´ibaadah na kujikurubisha kwa Allaah ambapo akawa amechukua mali ili iweze kumsaidia kumuabudu Allaah, basi hili linafaa, ni halali na ni chumo zuri.

[1] Allaah (Ta´ala) amesema:

”Atakayemkufuru Allaah baada ya kuamini kwake [atachukuliwa hatua] – isipokuwa yule aliyelazimishwa na huku moyo wake ukawa umetua juu ya imani. Lakini aliyekifungulia ukafiri kifua chake, basi hao watapata ghadhabu kutoka kwa Allaah na watapata adhabu kubwa. Hivyo kwa sababu wao wamefadhilisha maisha ya dunia kuliko ya Aakhirah na kwamba Allaah hawaongoi watu makafiri.”(an-Nahl 16:106)

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Nawaaqidh-il-Islaam http://ajurry.com/safrawy/chorohat-elakida/chorohat-nawakid-elislam/charh-salah-fawzan/01.mp3
  • Imechapishwa: 03/08/2018