Kichinjwa cha kwenye maulidi haifai kukila

Swali: Je, inajuzu kula nyama iliyochinjwa kwenye maulidi ya Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) au maulidi nyinginezo?

Jibu: Vyenye kuchinjwa kwenye maulidi ya Mtume au walii kwa ajili ya kumuadhimisha ni katika vilivyochinjwa kwa ajili ya asiyekuwa Allaah, jambo ambalo ni shirki. Haijuzu kuila. Imethibiti kuwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

”Allaah amemlaani mwenye kuchinja kwa ajili ya asiyekuwa Allaah.”

  • Mhusika: al-Najnah ad-Daaimah
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaa al-Najnah ad-Daaimah (01/135)
  • Imechapishwa: 06/10/2020