Swali 174: Wale wanaomchinjia maiti wakati anapokufa – je, kitendo hichi ni Sunnah au si Sunnah?

Jibu: Ikiwa ni kwa jina la swadaqah hakuna neno kufanya hivo – Allaah akitaka. Ama ikiwa ni kwa imani fulani au kwa ajili ya kujifakhari na kwamba asiyechinja anaonekana duni mbele ya macho ya watu au kwa imani ya kwamba maiti huyu ananufaisha na anadhuru [haijuzu]. Ama ikiwa ni kwa njia ya swadaqah kwa wale waliokuja hakuna neno. Hadiyth inayosema kuwatengenezea familia ya Ja´far chakula na kwamba wamefikiwa na jambo lenye kuwashughulisha ni dhaifu ambayo haikuthibiti.

  • Mhusika: ´Allaamah Muqbil bin Haadiy al-Waadi´iy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Ijaabatu as-Saa-il, uk. 351
  • Imechapishwa: 17/09/2019