Swali: Ni ipi dalili juu ya kuharibika kwa swalah kwa yule mwenye kucheka japokuwa itakuwa ni kidogo au hata kama itakuwa ni kwa kucheka sana?

Jibu: Hili ni batili na linapatikana kwa Ahnaaf. Wanaona kuwa ikiwa mtu atapiga kicheko ndani ya swalah basi wudhuu´ na swalah yake vinaharibika. Kuhusu swalah kuharibika ni kweli. Kwa sababu hili ni kama mfano wa kunywa, kula, kuongea na kucheka. Ama ikiwa ni kutabasamu hakuna neno. Lakini kupiga kicheko kunaharibu swalah. Kwa sababu kupiga kicheko ni kubaya zaidi kuliko kuongea. Mtu anapopiga kicheko anatokwa na baadhi ya herufi. Wanachuoni wanasema mtu akiongea na akatokwa na herufi mbili basi swalah yake inabatilika. Vipi ikiwa atapiga kicheko?

  • Mhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah ar-Raajihiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaa Mutanawwi´ah (05) http://audio.islamweb.net/audio/index.php?page=FullContent&audioid=191110#219240
  • Imechapishwa: 11/09/2018