Swali: Je, imamu akatazwe akikomeka tu juu ya khutbah moja ya swalah ya ´iyd na anapata dhambi?

Jibu: Ndio, anatakiwa kukemewa kwa sababu ni kitendo kinachopingana na Sunnah. Baadhi ya wanafunzi, watu wanaojifanya na wao ni wanachuoni na wanaoanza kusoma hivi sasa pale tu wanapopata maoni fulani, basi wanayaweka hadharani na kuwashawishi watu. Lazimiana na yale wanayofanya watu katika mji na usiwashawishi watu. Usijionyeshe nafsi yake kwamba ni mwanachuoni na kwamba umevumbua kitu kisichojulikana na wengine. Yote haya ni katika ujinga. Haijuzu kuwashawishi watu wala kwenda kinyume na yale matendo waliyomo watu katika nchi.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh ´Umdat-il-Fiqh (14) https://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/Umdah-03-11-1434.mp3
  • Imechapishwa: 03/06/2019