Khutbah ya ´Iyd kabla ya swalah ni Bid´ah

Swali: Ni ipi hukumu ya kutanguliza Khutbah ya ´Iyd kabla ya swalah?  Ni ipi hukumu ya kuhudhuria Khutbah ya ´Iyd? Je, ni sharti juu ya kusihi kwa swalah?

Jibu: Kutanguliza Khutbah ya ´Iyd kabla ya swalah ni Bid´ah iliyokomewa na Maswahabah (Radhiya Allaahu ´anhum).

Kuhusu kuhudhuria sio jambo la wajibu. Mwenye kutaka ahudhurie, asikilize na kunufaika. Mwenye kutaka aondoke zake.

Kuhudhuria sio sharti juu ya kusihi kwa swalah ya ´Iyd. Sharti siku zote hutanguliza kabla ya kile kitendo chenye kushurutishwa ilihali Khtubah ni yenye kutolewa baada ya swalah.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (16/249-250)
  • Imechapishwa: 14/06/2018