Khutbah inatolewa na mwengine, na swalah ya ijumaa inaswalishwa na mwengine

Swali: Je, ni sahihi Khutbah ikatolewa na mwengine na swalah akaswalishwa na mwengine?

Jibu: Ndio. Inafaa akakhutubu mmoja na mwengine akaswalisha. Hakuna neno kufanya hivo. Hata hivyo lililo bora ni huyohuyo aliyetoa Khutbah ndiye aswalishe.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh ´Umdat-il-Fiqh (13) http://alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/umdah%20Fiqh-26-10-1434.mp3
  • Imechapishwa: 21/10/2017