Swali: Je, kutoka na Jamaa´at-ut-Tabliygh kunahesabika ni katika njia ya Allaah? Je, mfumo wao umejengwa juu ya njia ya Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) na as-Salaf as-Swaalih?

Jibu: Kutoka huku  kumezuliwa. Hakuna dalili juu yake. Kule kutoka nao kwa muda maalum na kuona kuwa ni katika mfumo wa Da´wah ni mfumo uliyozuliwa usiyokuwa na dalili. Ni wajibu kwa mtu asichukue maoni wala mifumo isipokuwa tu pale inapokuwa na dalili kutoka katika Qur-aan na Sunnah.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://www.youtube.com/watch?v=oMoaMLGx4k0
  • Imechapishwa: 12/11/2017