Maoni sahihi ambayo wamefikia wanachuoni wahakiki ni kwmaba Ilyaas na Khidhr wamekufa  na kwamba hakuna mtu yeyote aliye katikati baina ya Allaah na viumbe wake katika ruzuku, uumbaji, uongofu na nusura. Mitume ni wakati na kati katika baina ya Muumba na viumbe inapokuja katika kufikisha ujumbe. Hakuna namna yoyote ya kufikia furaha isipokuwa kwa kuwatii Mitume.

Ama kuhusu uumbaji, ruzuku, uongofu na nusura yake, hakuna awezaye kuyaendesha hayo isipokuwa Allaah. Haya hayahusiani kabisa na uhai wa Mitume. Bali hata nusura na ruzuku haitokamani na uhai wa Mitume.

  • Mhusika: Shaykh-ul-Islam Ahmad bin Taymiyyah
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Minhaaj-us-Sunnah an-Nabawiyyah (1/96-97)
  • Imechapishwa: 10/12/2018