al-Khadhir alikuwa akifuata dini gani?

Swali: al-Khadhir alikuwa akifuata dini gani? Ni Mtume yupi aliyekuwa akimfuata?

Jibu: Ametakasika Allaah. Alikuwa anafuata dini ya Uislamu wenye maana ya ujumla ambapo ni kujisalimisha kwa Allaah kwa kumpwekesha. Mitume wote walikuwa juu ya Uislamu. Wafuasi wao walikuwa juu ya Uislamu wenye maana ya kumnyenyekea Allaah (Subhaanahu wa Ta´ala). Uislamu umewakusanya Mitume wote; wote walikuwa juu ya Uislamu. Kwa msemo mwingine walikuwa ni wenye kujisalimisha na kumtakasia ´ibaadah Allaah (´Azza wa Jall). Uislamu katika kila wakati maana yake ni kumwabudu Allaah kwa yale aliyoyaweka katika Shari´ah katika wakati huo. Huu ndio Uislamu.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Nawaaqidh-il-Islaam (09) http://ajurry.com/safrawy/chorohat-elakida/chorohat-nawakid-elislam/charh-salah-fawzan/09.mp3
  • Imechapishwa: 24/03/2019