Khawaarij wakaaji ni wepi?


Swali: Nini maana ya “Khawaarij wakaaji”?

Jibu: Khawaarij wakaaji ni wale Khawaarij wasiopigana. Wao wanafanya uasi kwa maneno kwa aina ya kwamba wanasema maneno yanayowatoa katika mfumo wa Ahl-us-Sunnah wal-Jamaa´ah. Wanafanya uasi kwayo dhidi ya mtawala. Hawa ndio Khawaarij wakaaji. Kuhusu wale wanaopigana hawa ni wabaya zaidi kuliko wale wakaaji.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Haqiyqatu Da´wat-ish-Shaykh Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab http://alfawzan.af.org.sa/ar/node/17206
  • Imechapishwa: 01/01/2018