Swali: Khawaarij wa leo wamekuwa na nguvu katika baadhi ya miji. Je, wao ndio wanazingatiwa kuwa watawala katika miji hiyo kwa hoja ya kwamba mambo yao yametulia na kufanikiwa kwa nguvu…

Jibu: Mambo yao hayajafanikiwa na kutulia. Hawana utulivu wowote. Pindi mambo yao yatakuwa safi watu wa kwanza wataoanza kuwaua ni Waislamu na wale wenye kufuata haki na uongofu. Wakati watapojidhatiti vizuri wataanza na wao. Wao sio Ahl-ul-Hall wal-´Aqd ambao wameshika uongozi kwa nguvu. Wanapeana na kuchukua. Wanaua na kuuawa. Wao sio watawala. Ni waasi wanaotakiwa kusafishwa. Waislamu wanawaangalia Waislamu na wanawachukia makafiri wakati watu hawa wanawachukia na kuwadhuru Waislamu na kuwasalimisha makafiri.

  • Mhusika: ´Allaamah ´Abdul-Muhsin bin Hamad al-´Abbaad
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: http://www.sahab.net/forums/index.php?showtopic=148607f
  • Imechapishwa: 02/05/2018