Khawaarij wa leo ni Mujaahiduun?


Swali: Ni ipi nasaha yako kwa wale walioathirika na Khawaarij wa leo, wanawatetea na wanawaita kuwa ni “Mujaahiduun”? Watu hawa hawawafuati wanachuoni wakubwa na nasaha zao…

Jibu: Ni wajibu kwa mtu kumcha Allaah juu ya nafsi yake na atahadhari asije akatumbukia kwenye mambo ambayo yatakuja kumwangamiza na kumpoteza. Ni kweli ya kwamba watu hawa ni Mujaahiduun, lakini ni Mujaahiduun katika njia ya Shaytwaan. Ni Mujaahiduun katika njia ya Shaytwaan. Mtu awe tahadhari asidanganyike na watu hawa na kuwasema vibaya Ahl-ul-Haqq na wanachuoni wenye kubainisha haki.

  • Mhusika: ´Allaamah ´Abdul-Muhsin bin Hamad al-´Abbaad
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: http://www.sahab.net/forums/index.php?showtopic=148608
  • Imechapishwa: 02/05/2018