Swali: Kuna mafungamano yepi kati ya Khawaarij wa leo na kitabu “ad-Durar as-Saniyyah”?

Jibu: Kitabu “ad-Durar as-Saniyyah” kimeandikwa kwa mujibu wa madhehebu ya Ahl-us-Sunnah wal-Jamaa´ah kutokana na kulingania katika dini ya Allaah na kubainisha Tawhiyd na shirki. Khawaarij hawana mafungamano yoyote nacho. Khawaarij ni wenye kupuuzia elimu sahihi na wanachuoni na vitabu sahihi. Wanavipuuzia. Ni wenye kujiweka navyo mbali. Wameridhika na ufahamu wao wenyewe na ufahamu wa viongozi wao. Hawana mfumo uliyomo kwenye “ad-Durar as-Saniyyah”. Huu ni uongo.

“ad-Durar as-Saniyyah” haiamrishi uasi.

“ad-Durar as-Saniyyah” haimrishi kuwapuuza wanachuoni.

“ad-Durar as-Saniyyah” haimrishi kujiunga na Khawaarij.

Haimrishi haya. Inaamrisha kinyume na haya.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Fath-il-Majiyd (24) http://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/fathulmajid%207%20-%20… Toleo la: 22.05.2015
  • Imechapishwa: 11/02/2017