Swali: Ni ipi hukumu ya usahihi wa maneno yanayosema kwamba swalah ya ambaye nguo yake inavuka kongo mbili za miguu kuna khatari isikubaliwe? Je, huyu dhambi yake inakuwa kubwa zaidi kuliko ambaye anakula ribaa, mzinzi na mwenye kuwaasi wazazi wake? Tunataraji kuwekewa wazi na Allaah akujaze kheri.

Jibu: Wanachuoni wengi wanaona kuwa swalah ya ambaye nguo yake inavuka kongo mbili za miguu akiswali swalah yake haikubaliwi. Kwa sababu ameswali kwa nguo ambayo ni haramu kwake. Lakini hata hivyo maoni yenye nguvu kwamba ni kwamba swalah yake ni yenye kukubaliwa pamoja na kuwa anapata dhambi.

Ama kumlinganisha kati yake na kuwa na utovu kwa wazazi wawili na kuwakata ndugu ni jambo lisiloyumkinika. Kwa sababu mambo haya Allaah (´Azza wa Jall) ameyatishia. Mathamanisho ya nguo na adhabu ni jambo liko kwa Allaah (´Azza wa Jall).

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Liqaa´ ash-Shahriy (74) http://binothaimeen.net/content/1728
  • Imechapishwa: 24/08/2020