Kazi ya uja ni moja ya sifa zake kuu Mtume (صلى الله عليه وسلم)


Allaah (´Azza wa Jall) amesema:

وَإِن كُنتُمْ فِي رَيْبٍ مِّمَّا نَزَّلْنَا عَلَىٰ عَبْدِنَا فَأْتُوا بِسُورَةٍ مِّن مِّثْلِهِ وَادْعُوا شُهَدَاءَكُم مِّن دُونِ اللَّـهِ إِن كُنتُمْ صَادِقِينَ

“Mkiwa mko katika shaka kutokana na Tuliyoyateremsha juu ya mja Wetu, basi leteni Suurah mfano wake na waiteni mashahidi wenu pasipo na Allaah mkiwa ni wakweli.”[1]

Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) kusifiwa kwamba ni mja katika nafasi tukufu kama hii ni dalili inayoonyesha kwamba sifa yake kubwa (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ni kutekeleza kazi yake ya uja ambayo hakuna yeyote anayemfika katika wale viumbe wa mwanzo na wale waliokuja baadaye. Ni kama ambavo alisifiwa kazi yake ya uja katika mazingia ya kumsafirisha usifu pale aliposema:

سُبْحَانَ الَّذِي أَسْرَىٰ بِعَبْدِهِ لَيْلًا

”Utakasifu ni wa ambaye Alimsafirisha usiku mja Wake… “[2]

Vilevile katika mazingira ya kuteremsha pale aliposema:

تَبَارَكَ الَّذِي نَزَّلَ الْفُرْقَانَ عَلَى عَبْدِهِ

“Ametukuka Yule ambaye amemteremshia Pambanuo mja Wake.”[3]

[1] 02:23

[2] 17:01

[3] 25:25

  • Mhusika: ´Allaamah ´Abdur-Rahmaan bin Naaswir as-Sa´diy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Taysiyr-ul-Kariym, uk. 35
  • Imechapishwa: 22/05/2020