Kazi inamshughulisha kujifunza elimu na swalah

Swali: Mimi nina kazi nyingi ambazo zinanifanya kutafuta riziki. Kazi hizo zinanishughulisha kutokamana na kujifunza elimu yenye manufaa. Kazi hii wakati mwingine inafikia kunishughulisha wakati wa swalah yangu kufikiria. Je, mimi nitaadhibiwa kwa sababu ya kazi hii?

Jibu: Kuhusu kazi kukushughulisha kutokamana na kujifunza elimu hakuna neno. Kwa sababu kutafuta elimu ni faradhi yenye kutosheleza; wakijifunza baadhi ya watu dhambi haziwapati wengine. Kuhusu kazi kukushughulisha kutokamana na swalah, sikiliza maneno ya Allaah (Ta´ala):

يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا لَا تُلْهِكُمْ أَمْوَالُكُمْ وَلَا أَوْلَادُكُمْ عَن ذِكْرِ اللَّـهِ ۚ وَمَن يَفْعَلْ ذَٰلِكَ فَأُولَـٰئِكَ هُمُ الْخَاسِرُونَ

“Enyi walioamini! Zisikushughulisheni mali zenu na wala watoto wenu mkaacha kumtaja Allaah. Na yeyote atakayefanya hivyo, basi hao ndio waliokhasirika.”[1]

Usikhasirike! Jaribu uuhudhurishe moyo wako kama ulivyouhudhurisha mwili wako ndani ya swalah na usijishughulishe na mengineyo. Izoweze nafsi yako juu ya hili mpaka uweze kuhisi ladha ya swalah na ili swalah yako iwe ni yenye kukukataza kutokamana na machafu na maovu.

[1] 63:09

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Liqaa´ ash-Shahriy (65) http://binothaimeen.net/content/1468
  • Imechapishwa: 05/06/2020