Kazi ambayo mkurugenzi ni mwanamke


Swali: Mimi nafanya kazi katika dula la dawa na mmiliki wa duka amemfanya mkurungezi juu yetu ni mwanamke. Unaninasihi nini?

Jibu: Nakunasihi usibaki katika duka hili la dawa. Jihadhari na tafuta kazi nyingine. Nakupa bishara njema kwa sababu Allaah (Subhaanah) amesema:

وَمَن يَتَّقِ اللَّـهَ يَجْعَل لَّهُ مَخْرَجًا وَيَرْزُقْهُ مِنْ حَيْثُ لَا يَحْتَسِبُ

“Na yule anayemcha Allaah humjaalia njia [ya kutokea] na atamruzuku kutoka njia ambayo hatizamii.”[1]

Ukiweza kumnasihi mmiliki wa duka ili ateue mkurugenzi mwanamme basi fanya hivo. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Dini ni kupeana nasaha.”

[1] 65:02-03

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (09/39)
  • Imechapishwa: 09/07/2021