Kauli yenye nguvu ni kuwa mwanamke kuonesha uso wake ni haramu


Uzuri wa mwanamke uko usoni mwake. Kauli yenye nguvu ambayo imeegemea katika dalili ni kuwa, ni Haramu kwake kutoka ikiwa bado angali ni mjane. Ama kama ameshakuwa mzee, kapewa rukhusa ya hilo. Anasema Allaah (Subhaanahu wa Ta´ala):

وَالْقَوَاعِدُ مِنَ النِّسَاءِ اللَّاتِي لَا يَرْجُونَ نِكَاحًا فَلَيْسَ عَلَيْهِنَّ جُنَاحٌ أَن يَضَعْنَ ثِيَابَهُنَّ غَيْرَ مُتَبَرِّجَاتٍ بِزِينَةٍ ۖ وَأَن يَسْتَعْفِفْنَ خَيْرٌ لَّهُنَّ

“Na Al-Qawaa’id (wanawake wazee wasiozaa tena au kutokwa hedhi) miongoni mwa wanawake ambao hawataraji kuolewa, basi hakuna ubaya juu yao kupunguza baadhi ya nguo zao bila ya kuonyesha mapambo yao (au kujishaua). Na kama wakijisitiri (kwa kujifunika vyema) ni kheri kwao.” (24:60)

Ikiwa ni mama mwenye umri mkubwa na wala hakuogopwi kwake kufitinisha watu, lau atatoka na uso wake kaufunua, hakuna neno kwa hilo.

  • Mhusika: ´Allaamah Muqbil bin Haadiy al-Waadi´iy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: http://muqbel.net/fatwa.php?fatwa_id=1203
  • Imechapishwa: 03/03/2018