Katwaharika na hedhi lakini daktari kamkataza kukoga

Swali: Kuna mwanamke mgonjwa aliyekuwa na hedhi sasa katwaharika. Afanye nini baada ya kutwahirika naye amekatazwa kukoga?

Jibu: Baada ya kukatika damu yake atatayamamu. Mgonjwa akikhofia maradhi yake yasizidi au kudumu, Allaah Kajaalia kutayamamu badala ya kutia Wudhuu (kwa maji).

  • Mhusika: ´Allaamah Muqbil bin Haadiy al-Waadi´iy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: http://muqbel.net/fatwa.php?fatwa_id=450
  • Imechapishwa: 04/03/2018