Swali:  Katika mji wetu kuna mapote na uchaguzi. Je, inajuzu kwetu kushiriki ili tuweze kuchagua aliye afadhali na mwenye madhara khafifu katika dini yetu.

Jibu: Haya sio katika Uislamu. Katika Uislamu hakuna uchaguzi. Katika Uislamu kiongozi anachaguliwa kwa bay´ah ya Ahl-ul-Hall wal-´Aqd[1] miongoni mwa raia ambao ni wanachuoni na watu wenye mamlaka katika nchi. Waliobaki wanawafuata Ahl-ul-Hall wal-´Aqd. Haya ndio mafunzo ya Uislamu na hakuna uchaguzi. Hii ni nidhamu isiyokuwa ya Kiislamu.

[1] Tazama https://firqatunnajia.com/ni-kina-nani-ahl-ul-hall-wal-aqd-wanaomteau-mtawala/

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: at-Tafsiyr al-Mufasswal (79) http://www.alfawzan.af.org.sa/node/13596
  • Imechapishwa: 22/08/2020