Katika Sunnah kumethibiti Takbiyr iliyofungamanishwa?

Swali: Katika Sunnah kumethibiti Takbiyr iliyofungamanishwa (Muqayyad)?

Jibu: Takbiyr iliyofungamanishwa kwa mujibu wa wanachuoni inakuwa baada ya zile swalah tano. Kuanzia siku ya ´Arafah mpaka ile siku ya mwisho ya Tashriyq. Mtu anatakiwa kuleta Takbiyr siku ya ´Arafah, siku ya ´Iyd na yale masiku matatu ya Tashriyq. Kwa mwenye kuhiji ni pindi atapohudhuria ile siku ya kuchinja atakaporusha mawe kwenye nguzo ya ´Aqabah. Hii ndio Takbiyr iliyofungamanishwa. Imechukuliwa katika maneno Yake (Ta´ala):

وَاذْكُرُوا اللَّـهَ فِي أَيَّامٍ مَّعْدُودَاتٍ

”Mtajeni Allaah katika siku za kuhesabika.”[1]

[1] 02:203

  • Mhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah ar-Raajihiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaa Mutanawwi´ah (08) http://audio.islamweb.net/audio/index.php?page=FullContent&audioid=191309#219638
  • Imechapishwa: 20/01/2019