Katika mirathi mwanamke anagawiwa sawa kama mwanaume?


Swali: Mtu akiwaachia warithi wake mali baada ya kufa kwake. Je, mali hiyo itagawiwa kati yao sawa sawa mwanamke apewe kama mwanaume?

Jibu: Hapana. Wapewe kama jinsi Allaah Alivyowagawia:

لِلذَّكَرِ مِثْلُ حَظِّ الْأُنثَيَيْنِ

”Mwanamume atastahiki mfano wa fungu la wanawake wawili.” (04:11)

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Zaad-il-Ma´aad (43) http://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/mo--1432-03-17.MP3
  • Imechapishwa: 16/11/2014