Katika hali hizi ni kafiri bila ya shaka

Swali: Ni ipi tafsiri sahihi ya maneno ya Allaah (Subhaanah):

وَمَن لَّمْ يَحْكُم بِمَا أَنزَلَ اللَّـهُ فَأُولَـٰئِكَ هُمُ الْكَافِرُونَ

“Na yeyote asiyehukumu kwa yale aliyoyateremsha Allaah, basi hao ndio makafiri.” (05:44)

Jibu: Wanachuoni wameifafanua. Rejeeni katika tafsiri ya Ibn Kathiyr mtaona kuwa Aayah hii imefafanuliwa. Inategemea na hali ya mtawala.

Anaonelea kuwa ni halali hukumu kwa kanuni? Anaonelea kuwa kanuni ni bora kuliko hukumu ya Allaah? Anaonelea kuwa zote ni sawa? Anaonelea kuwa ana khiyari ya kuhukumu? Katika hali hizi huyu ni kafiri bila ya shaka.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh ´Umdat-il-Fiqh (01) http://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/omdh–14340126_0.mp3
  • Imechapishwa: 25/08/2020