Katika hali hii naweza kuikata swalah yangu na kujiunga na mkusanyiko?    

Swali: Nimekuja kuswali hapa nikakuta swalah tayari imekwisha ambapo nikawa nimeswali peke yangu. Katikati ya swalah kumekuja kundi la watu na wakakimu swalah. Katika hali hii nifanye nini pamoja na kujua kuwa nimeshaswali Rakaa´ moja peke yake?

Jibu: Mtu akiingia katika swalah peke yake na kukataka kuswaliwa mkusanyiko mwingine, katika hali hii ana khiyari baina ya mambo matatu:

La kwanza: Anaweza kuendelea na swalah yake, kwa kuwa ni mwenye kupewa udhuru.

La pili: Anaweza kuikata swalah yake ili ajiunge na mkusanyiko.

La tatu: Anuie kuwa ni ya Sunnah na aikhafifishe ili aweze kuwahi swalah ya mkusanyiko. Yote haya wanachuoni wameyajuzisha. Kwa hivyo una khiyari ukipenda unaweza kuendelea juu ya yale uliyomo, ukatoa Tasliym na kwenda zako, na ukipenda ukanuia kuwa ni ya Sunnah na ukaikhafifisha na ukaikamilisha Rakaa´ mbili kisha ukajiunga na mkusanyiko, na ukipenda vilevile unaweza kuikata na ni sawa kufanya hivo. Lakini kuhusu chaguo hili la mwisho huenda mtu akauliza ni vipi niikate ilihali ni faradhi ilihali faradhi haijuzu kuikata. Jibu ni kuwa mimi sikuikata kwa kuipuuza, lakini nimeikata ili niliendee lililo bora zaidi ambalo ni mkusanyiko.

Haijanidhihirikia hali iliyo bora zaidi. Lakini akiinuia ni ya Sunnah na akaikhafifisha ili asiipoteze swalah hii ni bora zaidi kuliko kuikata.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Liqaa’ ash-Shahriy (06)
  • Imechapishwa: 03/05/2020