Katika hali hii msafiri anatakiwa kuswali msikitini


Swali: Vipi msafari anaswali akibaki ndani ya mji chini ya siku nne? Aswali msikitini, ajumuishe swalah au afupishe?

Jibu: Ikiwa anasikia adhaana na yuko karibu na msikiti aswali pamoja na waislamu. Asiswali sehemu nyingine. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Atakayesikia adhaana na asiitikie basi hana swalah ikiwa hana udhuru wowote.” Kukaulizwa: “Ni udhuru upi?” Akasema: “Khofu au maradhi.”

Ambaye anasikia adhaana na yuko karibu na msikiti anatakiwa kuswali msikitini. Haijalishi kitu hata kama atakuwa ni msafiri. Anatakiwa kuswali kikamilifu na wao. Vilevile asijumuishe kwa sababu ni kama mkazi.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Tafsiyr-ish-Shaykh Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab (12) http://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/tf–1432-08-02.mp3
  • Imechapishwa: 02/06/2018