Katika hali hii mke halazimiki kutoa kafara


Swali: Je, ni lazima kwa mwanamke kutoa kafara kama mume wake amemlazimisha kufanya jimaa mchana wa Ramadhaan?

Jibu: Akilazimishwa ulazimisho kwa njia ya kwamba hakuwa na namna ya kumkwepa, halazimiki kutoa kafara. Amesema (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):

“Ummah wangu umesamehewa makosa, kusahau na yale waliyotenzwa nguvu kwayo.”

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Ighaathat-il-Lahfaan (96) https://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/igahthat-12021440h.mp3
  • Imechapishwa: 28/05/2019