Katika hali hii kunasomwa du´aa ya kufungulia swalah au al-Faatihah moja kwa moja?


Swali: Ninapoingia msikitini na nikamkuta imamu anasoma al-Faatihah nisome du´aa ya kufungulia swalah au hapana?

Jibu: Unapojiunga na imamu na ukamkuta imamu anasoma al-Faatihah, basi kati ya al-Faatihah na kusomwa kwa Suurah nyingine au kinyamazo – kama inavokuwa mara nyingi – tunakwambia kuwa unatakiwa sasa kunyamaza kwa sababu ya kisomo cha imamu. Atapomaliza kusoma al-Faatihah soma du´aa ya kufungulia swalah kisha ndio usome al-Faatihah hata kama imamu atakuwa anasoma.

Lakini ukichelea kuwa hatonyamaza kati ya al-Faatihah na kusoma Suurah nyingine au ukachelea atasoma Suurah fupi ambayo haitokuwezesha kusoma al-Faatihah, basi pale tu utapojiunga naye unatakiwa kusema “Allaahu Akbar” na useme:

أعوذ بالله من الشيطان الرجيم

“Najilinda kwa Allaah kutokamana na shaytwaan aliyefukuzwa.”

kisha ndio usome al-Faatihah. Kwa sababu Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alikataza mswaliji kusoma na huku imamu yuko anasoma isipokuwa tu al-Faatihah.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Liqaa' ash-Shahriy (40) http://binothaimeen.net/content/913
  • Imechapishwa: 22/09/2018