Katika hali hii kiapo hakifungiki

Swali: Kufanya uvuaji katika kiapo kwa utashi kunaondosha kafara?

Jibu: Mtu akisema “Ninaapa kwa jina la Allaah kwamba nitafanya kitu fulani – Allaah akitaka” au akasema “Ninaapa kwa jina la Allaah kwamba nitasafiri kesho – Allaah akitaka” kisha asifanye na wala asisafiri, basi kiapo hakifungiki. Kwa sababu amekifungamanisha na matakwa ya Allaah. Vivyo hivyo akisema “Ninaapa kwa jina la Allaah kwamba sintokula chakula cha fulani – Allaah akitaka” kisha akala chakula chake basi kiapo hakifunguki. Lakini asipokifungamanisha kiapo na matakwa na wala asitimize alichokiapia basi kinafungika na ni lazima kwake kutoa kafara.

  • Mhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah ar-Raajihiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaa Mutanawwi´ah (13) https://audio.islamweb.net/audio/index.php?page=FullContent&audioid=191589#219913
  • Imechapishwa: 21/02/2020