Katika hali hii chukua mali ya mumeo

Swali: Mwanamke kuchukua kutoka katika mali ya mumewe kwa ajili ya haja zake ni sharti apate idhini ya mume?

Jibu: Hapana, haikushurutishwa. Hind (Radhiya Allaahu ´anhaa) alisema: ”Ee Mtume wa Allaah! Hakika Abu Sufyaan ni mwanamme bakhili sana na wala hanipi mimi na wana wangu kinachotutosheleza isipokuwa kile ninachochukua kutoka katika mali yake pasi na yeye kujua. Je, napata dhambi?” Akasema (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):

”Chukua kutoka katika mali yake kwa wema kile kinachokutosheleza wewe na wanao pasi na idhini yake.”

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaad-ud-Duruus https://binbaz.org.sa/fatwas/6185/%D9%87%D9%84-%D9%8A%D8%AC%D9%88%D8%B2-%D8%A7%D8%AE%D8%B0-%D8%A7%D9%84%D9%85%D8%B1%D8%A7%D8%A9-%D9%85%D9%86-%D9%85%D8%A7%D9%84-%D8%B2%D9%88%D8%AC%D9%87%D8%A7-%D9%84%D8%AD%D8%A7%D8%AC%D8%AA%D9%87%D8%A7
  • Imechapishwa: 02/12/2020