Katika adhaana ipi mwadhini husema الصلاة خير من النوم?


Swali: Sentesi isemayo:

الصلاة خير من النوم

“Swalah ni bora kuliko usingizi.”

Inasemwa katika adhaana ya kwanza kabla ya Fajr au ni katika adhaana ya pili? Ni ipi dalili ya kusema hivo? Nini aseme mwenye kuyasikia baada ya muadhini?

Jibu: Sunnah ni kusema hivo katika adhaana ya mwisho, kama yalivyopokelewa hayo katika Hadiyth ya Abu Mahdhuurah. Imepokelewa dalili vilevile katika Hadiyth ya ´Aaishah (Radhiya Allaahu ´anhaa) kwamba mwadhini alikuwa akiyasema katika adhaana ya mwisho baada ya kuchomoza kwa alfajiri. Kisha baada ya hapo anasimama Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) na kuswali Rak´ah mbili na kutoka kwenda kuswali. Hayo ni baada ya adhaana ya kwanza ambayo ndio ile adhaana ya mwisho kwa nisba ya kile kinachoitwa adhanaa ya kwanza. Ni adhaana ya kwanza kwa nisba ya Iqaamah. Kwa sababu Iqaamah pia huitwa kuwa “adhaana”. Sunnah ni kusema hivo katika adhaana ya mwisho baada ya kuchomoza kwa alfajiri na adhaana hiyo ni ya kwanza kwa nisba ya Iqaamah. Ile adhaana ya kwanza inakuwa kwa ajili ya kuzindua. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema juu yake:

“Ili arudi aliyemacho katika nyinyi na imwamshe aliyelala katika nyinyi.”

Hii ni adhaana ya kuzindua ili aaamke yule aliyelala na arejee ambaye yumacho ili asirefushe swalah kwa sababu Fajr imekaribia.

Baadhi ya wanachuoni wameona kuwa mtu aseme hivo katika ile adhaana ya kwanza ambayo ndio mahali pa kuzindua kabla ya kuchomoza kwa alfajiri. Ni jambo lenye wasaa – Allaah akitaka. Hata hivyo mwadhini asisemi hivo katika adhaana zote mbili. Bora aseme hivo katika ile adhaana ya mwisho ambayo ndio ya kwanza kwa nisba ya Iqaamah. Nayo ni ile adhaana inayokuwa baada ya kuchomoza kwa alfajiri.

Mwenye kusikia hivo atasema mfano wake:

الصلاة خير من النوم

“Swalah ni bora kuliko usingizi.”

Hilo ni kutokana na maneno yake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):

“Mtapomsikia mwadhini basi semeni mfano wa anavosema.”

Mwenye kuitikia atasema:

الصلاة خير من النوم

“Swalah ni bora kuliko usingizi.”

Lakini wakati wa:

حي على الصلاة حي على الفلاح

“Njooni katika swalah! Njooni katika mafanikio.”

Atasema:

لا حول ولا قوة إلا بالله

“Hapana nguvu wala namna isipokuwa kwa msaada wa Allaah.”

Haya ndio yaliyowekwa katika Shari´ah. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alipokuwa akimsikia mwadhini akisema:

حي على الصلاة

“Njooni katika swalah!”

Anaitikia:

لا حول ولا قوة إلا بالله

“Hapana nguvu wala namna isipokuwa kwa msaada wa Allaah.”

Mwadhini akisema tena:

حي على الفلاح

“Njooni katika mafanikio.”

Anaitikia:

لا حول ولا قوة إلا بالله

“Hapana nguvu wala namna isipokuwa kwa msaada wa Allaah.”

Kwa sababu mtu hajui atapata nguvu za kufanya hivo au hatopata na hajui kama atakuwa na wepesi wa kufanya hivo au hatokuwa na wepesi huo. Kwa hiyo anatakiwa kusema:

لا حول ولا قوة إلا بالله

“Hapana nguvu wala namna isipokuwa kwa msaada wa Allaah.”

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Nuur ´alaad-Darb https://binbaz.org.sa/fatwas/7775/%D8%A7%D9%84%D8%B5%D9%84%D8%A7%D8%A9-%D8%AE%D9%8A%D8%B1-%D9%85%D9%86-%D8%A7%D9%84%D9%86%D9%88%D9%85-%D9%85%D8%AD%D9%84%D9%87%D8%A7-%D9%88%D9%85%D8%A7-%D9%8A%D9%82%D8%A7%D9%84-%D8%B9%D9%86%D8%AF-%D8%B3%D9%85%D8%A7%D8%B9%D9%87%D8%A7
  • Imechapishwa: 13/04/2020