Kasoro katika injini ya gari


Swali: Kuna mtu alinunua gari na baada ya masiku kadhaa ikambainikia kuwa gari hii ina kasoro katika injini ambayo ni kuhitajia mafuta kila wakati. Je, ana haki ya kurudisha kutokana na ulaghai?

Jibu: Ndio. Linaingia chini ya haki ya kurudisha kutokana na kasoro. Isipokuwa kama alikuwa amemuwekea sharti hapo kabla ya kwamba iko na kasoro na akaridhia kasoro hiyo, katika hali hiyo hana haki ya kurudisha.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh ´Umdat-il-Fiqh (28)
  • Imechapishwa: 29/01/2022