Kaburi kumbana mwanaadamu ni haki. Hakuna atayesalimika na hili. Litampitikia muislamu na asiyekuwa muislamu. Kafiri litambana mpaka mbavu zake zikutane. Kuhusu muumini kaburi pia litambana. Wanachuoni wamesema kaburi kumbana muislamu ni kama mfano wa mpenzi anapombana mpenzi wake. Ijapokuwa atahisi maumivu fulani, lakini hata hivyo ni kama mfano wa mpenzi anapombana kipenzi chake. Kwa msemo mwingine ni kwamba kaburi kumbana mwanaadamu ni jambo la haki. Lakini hata hivyo kwa muumini ni mbano wa mapenzi na kwa kafiri ni mbano wa chuki na adhabu.

  • Mhusika: Shaykh Swaalih bin ´Abdil-´Aziyz Aalish-Shaykh
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Lum´at-il-I´tiqaad, uk. 124
  • Imechapishwa: 27/08/2020