Wakati kuliposemwa kuambiwa Maalik bin Anas (Rahimahu Allaah):

”Ee Abu ´Abdillaah!

الرَّحْمَـٰنُ عَلَى الْعَرْشِ اسْتَوَىٰ

“Mwingi wa rehema amelingana juu ya ´Arshi.”[1]

Amelingana vipi?”

Maalik akaanza kutokwa na jasho na wasikilizaji wakasubiri wamsikie atasema nini. Akainua kichwa chake kisha akasema: ”Kulingana si kwamba ni jambo lisilofahamika na namna haitambuliki. Ni wajibu kuamini hilo na kuuliza juu ya hilo ni Bid´ah. Nakuona kuwa ni mtu muovu.” Akaamrisha atolewe nje.

Mwenye kupindisha kulingana (الإستواء) kwamba ni kutawala (الإستيلاء) basi atakuwa amejibu kinyume na yale aliyojibu Maalik (Rahimahu Allaah) na amepita njia nyingine. Jibu la Maalik (Rahimahu Allaah) kuhusu kulingana linatumiwa katika sifa zengine zote kama mfano wa kushuka, kuja, mkono, uso na nyenginezo. Hivyo mtu anatakiwa kusema kuhusiana na kushuka:

”Kushuka si kwamba ni jambo lisilofahamika na namna haitambuliki. Ni wajibu kuamini hilo na kuuliza juu ya hilo ni Bid´ah.”

Vivyo hivyo kuhusiana na sifa zengine zote kwa sababu kwani zina kazi moja kama mfano wa kulingana ambako kumetajwa katika Qur-aa na Sunnah.

[1] 20:05

  • Mhusika: Shaykh-ul-Islaam Ahmad bin Taymiyyah
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (4/4)
  • Imechapishwa: 28/03/2019