al-Ikhwaan al-Muslimuun wanapita juu ya kanuni hii waliyowekewa na yule mtu wa kwanza, nakusudia Hasan al-Bannaa. Kwa ajili hiyo hutowaona wakinasihiana jambo ambalo limetolewa kutoka katika Qur-aan na Sunnah. Miongoni mwazo ni Suurah “al-´Aswr”:

وَالْعَصْرِ إِنَّ الْإِنسَانَ لَفِي خُسْرٍ إِلَّا الَّذِينَ آمَنُوا وَعَمِلُوا الصَّالِحَاتِ وَتَوَاصَوْا بِالْحَقِّ وَتَوَاصَوْا بِالصَّبْرِ

“Naapa kwa al-‘Aswr. Hakika ya mwanaadamu bila ya shaka yumo katika khasara. Isipokuwa wale walioamini na wakatenda mema na wakausiana kwa kufuata ya haki na wakausiana kuwa na subira.”[1]

Suurah hii Maswahabah wa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) walipokuwa wanakutana kisha wakataka kutengana basi mmoja wao anamsomea mwengine Suurah hii kutokana na umuhimu wake:

وَتَوَاصَوْا بِالْحَقِّ وَتَوَاصَوْا بِالصَّبْرِ

“… wakausiana kwa kufuata ya haki na wakausiana kuwa na subira.”

Kama mnavyojua haki ni kinyume cha batili. Batili ina misingi na matawi yake. Kila kinachoenda kinyume na usawa ni batili. Ibara hii ndio sababu ya kubaki kwa al-Ikhwaan al-Muslimuun kwa karibu miaka sabini wakiwa mbali na kutendea kazi kuuelewa Uislamu ufahamu ambao ni sahihi. Kwa ajili hiyo wako mbali na kuutendea kazi Uislamu kimatendo. Kwa sababu asinacho hakuna atoacho.

[1] 103:01-03

  • Mhusika: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaa ´Ulamaa-ul-Kibaar fiy al-Irhaab wat-Tadmiyr, uk. 424
  • Imechapishwa: 19/01/2020