Nataka kuwapa kanuni khaswa wanafunzi: yakigongana maoni yanayosema kwamba kitu fulani kinafunguza na mengine yanayosema kwamba hakifunguzi ni yepi yenye nguvu zaidi? Ni yale yenye kusema kwamba hakifunguzi. Kwa sababu haifai kwetu kuharibu ´ibaadah ya Kishari´ah pasi na dalili ya Kishari´ah. Kwa sababu tukiharibu swawm basi tutakuwa tumemfanyia vibaya mfungaji huyu. Jengine ni kwamba tutakuwa tumesema juu ya Allaah tusichokijua. Kanuni ifahamu hivi katika kila kitu. Kila kunapogongana mambo mawili; moja linasema kuwa ni wajibu na lingine linasema kuwa sio wajibu, basi msingi ni kutokuwa wajibu. Jambo moja linasema kuwa ni haramu na lingine linasema kuwa sio haramu, basi msingi ni kutokuwa haramu. Jambo moja linasema kuwa linafunguza na lingine linasema kuwa halifunguzi, basi msingi ni kutofunguza.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Liqaa´ ash-Shahriy (71) http://binothaimeen.net/content/1624
  • Imechapishwa: 24/03/2020