Kanuni ambayo Mumayyi´ah wanataka kuitokomeza


Kuna watu wanaotaka kuibadili kanuni hii ya kwamba rafiki anaathiri na kwamba mtu anakuwa kama wale anaotangamana nao. Wanasema kuw wanaweza kuiendesha mioyo yao. Si sahihi. Hawaendeshi nyoyo zao wala hawamiliki kugeuka kwake. Salaf walilitambua hili. Ndio maana walikuwa ni wenye kupupia juu ya nyoyo zao na wanaotaamiliana nao. Wakati jitu limoja la Bid´ah lilipotaka kumsomea Aayah ya Qur-aan Muhammad bin Siriyn, akakataa kumsikiliza na kumwambia:

“[Sitaki] hata Aayah moja.”

Muhammad bin Siriyn alikuwa ni mmoja katika maimamu wa Taabi´uun. Alikataa kumsikiliza mtu wa Bid´ah amsomee kitu katika Qur-aan. Mtu wa Bid´ah mwingine alimwendea Imaam Maalik na akamuomba aweze kumwambia kitu ambapo Maalik akasema kumjibu:

“[Sitaki] hata nusu ya neno.”

Wasio wasomi wamepatia pindi waliposema kuwa endapo maneno hayatoingia yote basi angalau kutaingia baadhi yake. Ni sahihi. Hii ina maana kwamba usijiaminishe. Endapo maneno hayatoingia yote basi angalau kutaingia baadhi yake.

  • Mhusika: ´Allaamah Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab al-Wasswaabiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: http://olamayemen.com/Dars-14107
  • Imechapishwa: 19/09/2020