Mwandishi (Rahimahu Allaah) anaanza kutaja dalili zenye kuonesha kuwa Allaah yuko juu ya ´Arshi. Kuna dalili tele. Tukienda kwa moja moja basi kuna dalili zinazopita elfu moja, kama alivyosema ´Allaamah Ibn-ul-Qayyim. Dalili hizi moja moja zina kanuni inazozikusanya. Tumetangulia kutaja baadhi yake. Miongoni mwa aina ya dalili alizotaja mwandishi ni zifuatazo:

Aina ya kwanza: Kila andiko lililosema kuwa Allaah amelingana juu ya ´Arshi, basi ni dalili yenye kufahamisha Ujuu. Dalili hizi zimetajwa sehemu saba katika Qur-aan:

Sehemu ya kwanza: Katika Suurah “al-A´raaf”. Amesema (Ta´ala):

إِنَّ رَبَّكُمُ اللَّـهُ الَّذِي خَلَقَ السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضَ فِي سِتَّةِ أَيَّامٍ ثُمَّ اسْتَوَىٰ عَلَى الْعَرْشِ

“Hakika Mola wenu ni Allaah ambaye ameumba mbingu na ardhi katika siku sita kisha akalingana juu ya ‘Arshi.” (07:54)

Sehemu ya pili: Suurah “Yuunus”. Amesema (Ta´ala):

إِنَّ رَبَّكُمُ اللَّـهُ الَّذِي خَلَقَ السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضَ فِي سِتَّةِ أَيَّامٍ ثُمَّ اسْتَوَىٰ عَلَى الْعَرْشِ ۖ يُدَبِّرُ الْأَمْرَ

“Hakika Mola wenu ni Allaah ambaye ameumba mbingu na ardhi katika siku sita kisha akalingana juu ya ‘Arshi. Anayaendesha mambo.” (10:03)

Sehemu ya tatu: Suurah “Twaaha”. Amesema (Ta´ala):

الرَّحْمَـٰنُ عَلَى الْعَرْشِ اسْتَوَىٰ

“Mwingi wa rehema amelingana juu ya ´Arshi.” (20:05)

Sehemu ya nne: Suurah “ar-Ra´d”. Amesema (Ta´ala):

اللَّـهُ الَّذِي رَفَعَ السَّمَاوَاتِ بِغَيْرِ عَمَدٍ تَرَوْنَهَا ۖ ثُمَّ اسْتَوَىٰ عَلَى الْعَرْشِ

“Allaah Ambaye ameinua mbingu bila ya nguzo mnaziona kisha akalingana juu ya ‘Arshi.” (13:02)

Sehemu ya tano: Suurah “al-Furqaan”. Amesema (Ta´ala):

ثُمَّ اسْتَوَىٰ عَلَى الْعَرْشِ ۚالرَّحْمَـٰنُ فَاسْأَلْ بِهِ خَبِيرًا

“Kisha akalingana juu ya ´Arshi. Mwingi wa Rahmah basi ulizia kuhusu khabari Zake.” (25:59)

Sehemu ya sita: Suurah “as-Sajdah”. Amesema (Ta´ala):

هُوَ الَّذِي خَلَقَ السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضَ فِي سِتَّةِ أَيَّامٍ ثُمَّ اسْتَوَىٰ عَلَى الْعَرْشِ

“Yeye Ndiye aliyeumba mbingu na ardhi katika siku sita kisha akalingana juu ya ‘Arshi.” (57:04)

Sehemu ya saba: Suurah “al-Hadiyd”. Amesema (Ta´ala):

هُوَ الَّذِي خَلَقَ السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضَ فِي سِتَّةِ أَيَّامٍ ثُمَّ اسْتَوَىٰ عَلَى الْعَرْشِ

“Yeye Ndiye aliyeumba mbingu na ardhi katika siku sita kisha akalingana juu ya ‘Arshi.” (57:04)

Sehemu zote hizi Allaah ameelezea kuwa amelingana juu ya ´Arshi. Amefuatisha kwa neno “´alaa” likifahamisha Ujuu. Hizi ni dalili saba ambazo zimefungamana na kanuni moja.

Miongoni mwa kanuni hizo vilevile ni kila andiko ambalo limetaja Ujuu linatoa dalili kuonyesha Ujuu wa Allaah. Amesema (Ta´ala):

وَهُوَ الْعَلِيُّ الْعَظِيمُ

“Naye yuko juu, ni mkuu.” (02:255)

سَبِّحِ اسْمَ رَبِّكَ الْأَعْلَى

“Sabihi jina la Mola wako aliye juu.” (87:01)

Kuna dalili nyenginezo nyingi zilizo na kanuni kama hii.

Aina ya pili: Kila andiko lililosema kuwa Allaah yuko mbinguni ni dalili yenye kuonesha kuwa Allaah yuko juu ya ´Arshi. Amesema (Ta´ala):

أَأَمِنتُم مَّن فِي السَّمَاءِ

“Je, mnadhani mko katika amani na Aliyeko mbinguni.” (67:16)

Aina ya tatu: Kila andiko lililotaja kuwa vitu vinapanda Kwake basi ni dalili yenye kuonesha kuwa Allaah yuko juu ya ´Arshi. Amesema (Ta´ala):

إِلَيْهِ يَصْعَدُ الْكَلِمُ الطَّيِّبُ

“Kwake pekee linapanda neno zuri.” (35:10)

Kupanda ni kutokea kwa chini kwenda juu.

Aina ya nne: Kila andiko lililotaja kunyanyua ni dalili yenye kuonesha Ujuu wa Allaah (Ta´ala). Amesema (Ta´ala):

بَل رَّفَعَهُ اللَّـهُ إِلَيْهِ

“Bali Allaah alimnyanyua Kwake.” (04:158)

إِلَيْهِ يَصْعَدُ الْكَلِمُ الطَّيِّبُ

“Kwake pekee linapanda neno zuri.” (35:10)

Kunyanyua kunakuwa kutokea kwa chini kwenda juu.

Aina ya tano: Kila andiko lenye kutaja kushuka kutoka Kwake ni dalili yenye kuthibitisha Ujuu. Amesema (Ta´ala):

حم تَنزِيلُ الْكِتَابِ مِنَ اللَّـهِ الْعَزِيزِ الْحَكِيمِ

“Haa Miym. Ni uteremsho wa Kitabu kutoka kwa Allaah, Mwenye nguvu kabisa, Mwenye hikmah.” (45:02)

مُنَزَّلٌ مِّن رَّبِّكَ بِالْحَقِّ

“Kimeteremshwa kutoka kwa Mola wako kwa haki.” (06:114)

Kushuka kunakuwa kwa kutokea juu kwenda chini.

Aina ya sita: Kila andiko ambalo kunauliziwa “Allaah yuko wapi?” ni dalili yenye kuonesha Ujuu wa Allaah. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alisema kumuuliza mjakazi:

“Allaah yuko wapi?” Akajibu: “Mbinguni.” Akasema (´alayhis-Salaam): “Mwache huru! Kwani hakika ni muumini.”” Baada ya hapo akashuhudia kuwa ni muumini.”

Aina ya saba: Kuwafanya baadhi ya viumbe kuwa Kwake pasi na wengine. Amesema (Ta´ala):

وَلَهُ مَن فِي السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضِ ۚ وَمَنْ عِندَهُ لَا يَسْتَكْبِرُونَ عَنْ عِبَادَتِهِ

“Na ni Wake pekee wote waliomo katika mbingu na ardhi na wale walio Kwake hawatakabari na ‘ibaadah Yake.” (21:19)

Makusudio ya:

وَمَنْ عِندَهُ

“… na wale walio Kwake.”

bi maana walioko Kwake juu. Lau makusudio ya “Kwake” ingelikuwa ni ardhini, kama wanavyosema Jahmiyyah, basi kusingelikuwa faida yoyote ile ya umaalum huu. Allaah angelikuwa ardhini – kama wanavyodai – basi ingelikuwa viumbe wote walioko ardhini na mbinguni wako Kwake. Lakini badala Yake amesema:

وَلَهُ مَن فِي السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضِ

“Na ni Wake pekee wote waliomo katika mbingu na ardhi.”

Kisha akasema:

وَمَنْ عِندَهُ

“… na wale walio Kwake… “

Nao ni Malaika walioko juu.

لَا يَسْتَكْبِرُونَ عَنْ عِبَادَتِهِ

“… hawatakabari na ‘ibaadah Yake.”

Alipofanya baadhi ya viumbe kuwa Kwake pasi na wengine ni dalili tosha yenye kufahamisha kuwa makusudio ni Ujuu. Asingelikusudia Ujuu, basi ingelikuwa Malaika, mbingu na ardhi vyote viko Kwake. Lakini amefanya umaalum kwa baadhi ya viumbe ya kwamba wako Kwake. Hii ni dalili yenye kuonesha Ujuu.

Aina ya nane: Ameelezea utiifu kwa wale walioko Kwake katika Malaika. Amesema (Ta´ala):

إِنَّ الَّذِينَ عِندَ رَبِّكَ لَا يَسْتَكْبِرُونَ عَنْ عِبَادَتِهِ وَيُسَبِّحُونَهُ وَلَهُ يَسْجُدُونَ

“Hakika wale walioko kwa Mola wako hawatakabari kufanya ‘ibaadah Yake na wanamsabihi na Kwake pekee wanasujudu.” (07:206)

Maneno Yake:

إِنَّ الَّذِينَ عِندَ رَبِّكَ لَا يَسْتَكْبِرُونَ عَنْ عِبَادَتِهِ وَيُسَبِّحُونَهُ وَلَهُ يَسْجُدُونَ

“Hakika wale walioko kwa Mola wako.”

bi maana Malaika walioko juu ya mbingu.

  • Mhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah ar-Raajihiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh al-Qaa´idah al-Marraakushiyyah, uk. 41-44
  • Imechapishwa: 01/05/2020